Monday, March 21, 2016



Muimbaji wa ‘Bado’, Harmonize ameteuliwa kuwa balozi wa taasisi inayojihusisha na utunzaji wa mazingira, World Wide Fund for Nature – WWF kwa Tanzania.
Mkurugenzi wa WWF Tanzania, Dr. Amani Ngusaru akiwa na Harmonize baada ya kumteua rasmi kuwa balozi wa taasisi hiyo


Muimbaji huyo alisaini mkataba wa ubalozi huo wiki iliyopita kwenye ofisi za taasisi hiyo zilizopo Mikocheni, Dar es Salaam.

Kama sehemu ya ubalozi huo, Harmonize alihudhuria makabidhiano ya mradi wa maji unaotokana na nishati ya jua huko Kigamboni Jumamosi iliyopita.

Kabla ya Harmonize, ubalozi huo ulienda kwa Rich Mavoko.

0 comments:

Post a Comment