Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT, Mhe. Zitto Kabwe amejiuzulu ujumbe wake katika Kamati ya Huduma za Jamii kwa madai kuwa kuna uwezekano wa kuwepo katika vitendo vya rushwa katika kamati iyo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto amendika “Kuna tuhuma za rushwa dhidi ya Kamati mbalimbali za Bunge ikiwemo kamati ninayohudumu. Nimemwandikia Spika Kuomba Uchunguzi juu Ya tuhuma hizo na kwamba achukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayekutwa kuhusika na vitendo vya rushwa. Nimejiuzulu Ujumbe wa Kamati ili Kutoa Nafasi Ya Uchunguzi Husika.”
0 comments:
Post a Comment