Baba levo amefunguka hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha E News kinachorushwa na EATV Jijini Dar es salaam.
''Mimi spendi kusikia wamerudiana tena maana kila mara ni ugomvi wakipatanishwa ndani ya masaa machache tuu unasikia tena wamegombana na kupigana kabisa''-Amesema Baba Levo.
Aidha msanii huyo amebainisha kuwa moja ya mahusiano ya wasanii ambayo yanaonekana kuwa makini na kuonyesha njia ni yeye na mke wake, Peter Msechu na mke wake na msanii Jux na mpenzi wake Vanesa Mdee.

0 comments:
Post a Comment