Keri Hilson ni miongoni mwa wasanii wa kike ninaowaelewa na ukimya wake ulikuwa ukinisumbua sana.
Na sasa habari njema kwa mashabiki wake ni kuwa Miss Keri is back!
Kwa zaidi ya miaka mitano tangu aachie album yake ya mwisho, Keri Hilson ametangaza kurejea na album mpya, L.I.A.R. Album yake hiyo ya tatu, ni kifupi cha maneno, Love Is a Religion. Album zake za awali zilikuwa Perfect World, 2009 na No Boys Allowed ya mwaka 2010.
Kwenye album hiyo anadai ataeleza kinagaubaga kipi kilichotokea hadi akawa kimya na ameahidi kuwa hatokaa tena muda mrefu hivyo bila kutoa kazi. Wimbo wa kwanza kutoka kwenye album hiyo unaitwa, Again na utatoka Ijumaa hii. Umetayarishwa na Mike WiLL-Made It na kuandikwa na R. City.
L.I.A.R imepigwa tafu na Chris Brown, Polow Da Don, Timbaland, Danja na wengine.
Ikumbukwe pia kuwa mwaka huu Keri Hilson ndiye msanii aliyechaguliwa kama mentor kwenye Airtel Trace Music Star.

0 comments:
Post a Comment