Wednesday, March 30, 2016


Tukumbushane: Nyerere Na Wamarekani..

Ndugu zangu,

Unabaki kuwa ni ukweli wa kihistoria, kuwa mwaka 1964 ulikuwa ni mwaka mgumu sana kwa uongozi wa Julius Nyerere kuliko wakati mwingine wowote. Kulikuwa na matukio makubwa yaliyomtikisa Julius Nyerere na Tanzania kama taifa changa.

Tumeona mifano ya Mapinduzi ya Januari 12, Zanzibar na Army Mutiny ( Uasi wa jeshi) wa Januari 20, 1964.

Ni katika mwaka huo, Wachina na WaCuba waliingia kwa kasi Zanzibar mara baada ya Mapinduzi. Hali hii iliwatisha Wamarekani. Ikaja taarifa ya kupandikizwa ya kiintelijensia. Ni katika miezi hiyo hiyo. Kwamba Marekani na Uingereza wanapanga njama za kumwangusha Karume. Nyerere akaridhia Karume amfukuze Balozi Mdogo wa Marekani kutoka Unguja.

0 comments:

Post a Comment