Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wao uliofanyika Milenium Tower jijini Dar es salaam wakati alipoelezea kuhusiana na mkutano wa mwaka wa wadau wa LAPF unaotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa AICC mwezi huu kwa sikU mbili jijini Arusha. Pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama Bw. Valerian Mablangeti.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyotolewa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe wakati akizungumza nao katika ofisi za Shirika hilo zilizopo Mkumbusho jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama Bw. Valerian Mablangeti akiwafafanulia jambo waandishi wa habari wakati wa mkutano huo kulia ni Bw. James Mlowe Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF.
………………………………………………………………………………..
MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kuwa na sh.trioni moja na bilioni 87 za thamani ya uwekezaji kutoka mwezi juni mwaka jana.
MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kuwa na sh.trioni moja na bilioni 87 za thamani ya uwekezaji kutoka mwezi juni mwaka jana.
Hayo yalibainishwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF James Mlowe wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mkutano mkuu wa nane wa mfuko huo unaotarajiwa kufanyika Machi 10 na 11 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.
Alisema LAPF imeendelea kupiga hatua kila mwaka ukilinganisha na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii hapa nchini.
” LAPF imeweza kutoa mikopo ya masomo kwa watu 800 katika maeneo mbalimbali nchini yenye thami ya sh.bilioni 1.2 jambo ambalo tunajivunia” alisema Mlowe.
Akizungumzia kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika kwa wadau wa mfuko huo kupatiwa barua za mualiko.
Alisema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene na kuwa mawaziri wengine wakaoshiriki kwenye mkutano huo ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Jafo Selemani .
Alisema katika mkutano huo Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali atatoa taarifa ya hesabu za mfuko huo na pia kutakuwa na mada inayohusu afya kutoka kwa Daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
0 comments:
Post a Comment