Monday, March 21, 2016

Rais Mstaafu wa Tanzania Al Hajj Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika Kituo cha Kupigia Kura cha Miembeni Skuli ya Maandalizi akipokelewa na Sheha wa Miembeni. wakati wa zoezi la upigaji wa Kura za Marudio Zanzibar uliofanyila leo Zanzibar nzima kwa Nafasi za Urais wa Zanzibar, Uwakilishi na Udiwani. 
Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akipata maelekezo baada ya kukabidhiwa Karatasi za Kupigia Kura na Karani wa Kituo cha Kupigia Kura Skuli ya Maandalizi Miembeni Jimbo la Kikwajuni.
Rais Mstaafu wa Tanzania Al Hajj Ali Hassan Mwinyi akipiga kura yake katika Kituo cha Skuli ya Maandalizi Miembezi Zanzibar.
Rais Mstaafu wa Zanzibar Komando Dk Salim Amour Juma akiwasili katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi Jangombe Chekechea leo asubuhi kwa ajili ya kutimiza Haki yake ya Kidemokrasia ya Kumchagua Rais wa Zanzibar.

Rais Mstaafu wa Zanzibar Komandoo Dk Salmin Amour Juma akiwa na msaidizi wake akipiga Kura katika Kituo cha Skuli ya Maandalizi Jongombe Chekechea. 

Mama Fatma Karume akiongozana na Mjukuu wake Aisha Ali Karume wakiwasili katika Kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi Jangombe Zanzibar.

Mama Fatma Karume akisalimiana na Mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Slmin Amour Juma, Amini Salimin alipowasili katika Kituo cha Kupigia Kura cha Jimbo la Mpenda Skuli ya Maandalizi Chekechea leo asubuhi.  


Mama Fatma Karume akipiga kura yake  katika Kituo cha Kupigia Kura cha Jimbo la Mpenda Skuli ya Maandalizi Chekechea leo asubuhi.  

Balozi Ali Abeid Karume akiwa na Mke wakiwasili katika viwanja vya Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi Jangombe Chekechea kwa ajili ya kutimiza haki yao ya msingi ya kupiga Kura kumchagua Kiongozi wa Zanzibar. 

Balozi Ali Karume akipokea Kura kutoka kwa Karani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar alipofika katika Kituo hicho Kupiga kura yake leo asubuhi.

Balozi Ali Karume akipiga Kura yake Katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi 
Wananchi wa Shehia ya Kilimaniw akipiga Kura 

0 comments:

Post a Comment