Katika ukurasa wake wa Instagram Faiza ameandika huku akiwapondea wale wanaomsikitikia, na kusema kuwa Chid amejichagulia mwenyewe kuwa hivyo kwani kabla hajaanza kutumia alikuwa anafahamu madhara yake.
“Kila mtu anamsikitikia Chidi kwa nini? Chidi sio mtoto ni maisha aliyo chagua, pengine unaweza kumsikitia mtoto aliye jifunza akiwa chini ya miaka 18 lakini sio mtu mzima! Kila siku mifano tunaiona jinsi gani madawa yana haribu watu inaama hawaoni ? Hawasikii ?"Faiza ameendelea kuandika
"Hapana kwa kweli mimi naona unavuna unachokipanda. Unapo sema ugumu wa maisha ndiyo umekupeleka kuvuta madawa au kuuza - hivi mnazani wote tunao cheka maisha yetu mepesi? Kwa kweli ni uzembe......! acheni kabisa kuwahurumia watu kijinga, lazima wajue wamekosea sio kuwa peti peti”.
Pamoja na hayo Faiza ameonekana kuchukizwa na kitendo cha biashara ya madawa ya kulevya inayoendelea nchini, na kutaka watumiaji na wauzaji pia wafungwe iwapo watathibitika, ili kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya
“Hivi kwa nini wanao nunua madawa pia wasifungwe ??? Kwa sababu mtazamo wangu unaona mnunuzi na muuzaji wote ni wahalifu!
Kati ya hawa watu wawili wote wanafanya biashara maana kama hamna mnunuzi hakuna muuzaji, kama hakuna muuzaji hamna mnunuzi”, aliandika Faiza.
Pamoja na hayo Faiza amemtakia heri Chidi Benzi katika mapambano yake na kuachana na madawa ya kulevya, ili aweze kurudi kama zamani.

Nafikiri alichokiandika faiza kina ukweli kabisa,chid siyo mtoto mdogo ,chid ni kioo cha jamii chini wa mwamvuli wa usanii,hivyo anaushawishi mkubwa kwa jamii hasa kwa wapenzi wake . Vijana wengi wanatakiwa kumfata yeye katika Nyanja mbalimbali za kimaisha,sasa anapoamua kutumia nafasi aliyopewa na Mungu ya kuwa msanii kwa kuvuta unga,maana yake anataka kuwafundisha watoto wetu hasa wafuasi wake kubwia unga!.Hii ni kuidharirisha taaluma yake!
ReplyDeleteNdugu zangu wasanii,nyie kweli ni vioo vya jamii kama mmoja wenu afande sele alivyowahi kuimba katika moja ya nyimbo zake,mjitambue kwamba mnao ushawishi mkubwa sana chanya au hasi katika jamii.chochote kile msanii atakachoamua kikifanya ndani ya mwamvuli ya usanii,ajue kina madhara yake.
Naomba nitoe mfano mmoja, juzijuzi hapa msanii mmoja alitoka na staili ya kutembea kijotijoti,hehee! tulipata taabu kweli wazazi huko majumbani, unamwona mtoto anatembea ,ghafla kama anataka kuanguka ,wewe unastuka ukidhani kajikwaa,kumbe anatembea KIJOTIJOTI.Hii ni picha tosha ya kuonyesha jinsi gani msanii anaushawishi mkubwa ndani ya jamii.
Mimi si mshabiki sana wa mambo ya mziki,ila huwa naangalia kujua nini kinaendelea huko,kuna mwimbaji mmoja wa kizaire ( Kanda Bongo man). huyu jamaa alikuwa akipanda jukwaani utampenda kwa unadhifu yaani hata watu wakiiga uvaaji wake hasa unadhifu ,huna cha kulalamikia.
mwisho nawaomba wasanii wetu ,tumieni dirisha hilo la usanii katika kuleta mambo wenye ushawishi chanya katika jamii.Kuhusu ndugu yetu Chid ,tumuonyesheni upendo na kusaidia katika uamuzi wake wa sasa.