Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akiwa na Ali Kiba.
Yamekuwa
yakitokea mambo mengi kwenye uhusiano wa mastaa wawili Bongo, Jokate
Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Salehe Kiba ‘Ali Kiba’, mara wamwagane, mara
wazichape lakini safari hii inaonekana mwisho umefika, Ijumaa lina kitu
exclusive.
Hatua hiyo inakuja kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa,
Jokate amefunguka laivu kumchoka jamaa yake huyo akidai si mwanaume
anayeweza kumfikisha pale anapopataka.
Tujiunge na chanzo
Hivi
karibuni, rafiki wa karibu wa Jokate aliyeomba hifadhi ya jina lake
alieleza kuwa, uhusiano wa Kiba na Jokate umefika tamati kufuatia
malalamiko ambayo Jokate amekuwa akiyatoa akidai, staa huyo wa kibao cha
Nagharamia amekuwa haeleweki, hali inayosababisha mambo yao kutowaendea
vizuri.
Mwanamuziki Ali Salehe Kiba ‘Ali Kiba.
“Yaani
nyie hamjui tu lakini ukweli ni kwamba Jokate kamchoka Kiba kutokana na
mambo yake na ameamua sasa kuchukua hamsini zake, mwenyewe anasema
amekuwa akimshauri mambo mengi kuhusu maisha yao tena ya kimaendeleo
lakini Kiba amekuwa akiyapotezea.
“Jokate anasema, yeye ni
mwanamke mpambanaji hivyo anapokuwa na mwanaume, lazima awe
anayeshaurika lakini kwa Kiba imekuwa ni tofauti. Akishauriwa hili,
linaingilia huku na kutokea huku.
“Ukichanganya na haya madai yule
Sabby kuwa kuna sms zimenaswa akichati na Kiba ndiyo kabisaa shosti
wangu kachoka na kaamua kuwa na maisha yake,” alisema mtoa habari huyo.
Ni yaleyale ya kwa Diamond
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, Jokate anaona kama aliyokuwa akiyaona
kwa Diamond kipindi kile ndiyo anayokumbana nayo sasa, hivyo
anajitafakari upya aina ya wanaume wa kuwa nao kwenye uhusiano.
...Wakiwa kwenye pozi la mahaba.
“Yaani
yeye anachosema ni kwamba, haoni tofauti ya hawa wanaume wawili, Kiba
na Diamond na anavyoonekana si mtu wa kuja kuwa na mpenzi ambaye ni
mwanamuziki,” kilifunguka chanzo hicho.
JOKATE ANASEMAJE?
Baada ya kupata ubuyu huo, Ijumaa lilifanya jitihada za kuzungumza na
Jokate mwenyewe ambapo alipopatikana alifunguka kwa kifupi: “Hayo mambo
na Ali (Ali Kiba) yamenichosha, sasa nyie hicho mlichoambiwa andikeni
lakini mimi siwezi kuongea.Ijumaa: Angalau ufunguke kidogo sababu hasa
za kumchoka mshkaji ukiacha hizo ambazo tumeambiwa na chanzo.
Jokate: Sina la kusema.
Ijumaa: Au imekuuma kusikia anatoka na yule Sabby Angel? Funguka mama.
Jokate: Kama huyo Kiba anampenda sana huyo Sabby naamchukue kabisa, mimi nina maisha yangu sasa, halafu naomba mniache jamani!
Kiba kama kawa
Baada ya kumsikia Jokate a.k.a Kidoti, Ijumaa lilimvutia waya Kiba
lakini kama kawaida yake simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Jitahida za kumpata bado zinaendelea.
CHANZO: GPL
0 comments:
Post a Comment