Thursday, March 31, 2016


Msanii wa muziki wa bongo fleva miondoko ya Hip Hop Godzilla amesema katika mambo ambayo hapendi katika maisha ni kumnyooshea mtu kidole hasa pale anapofanya vibaya kwani hajui mtu huyo kesho yake itakuwaje

Msanii huyo ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha E News na kusisitiza kwamba kuna watu wanakuwa wanawanyooshea tuu watu vidole bila kujua kesho yake mtu huyo huyo anaweza kufanya kitu kikubwa zaidi.
''Mimi ukinikosea nafanya mambo yangu nikiamini siku moja utanikubali tuu''-Ameongeza Godzilla.
Aidha Msanii huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ''I get High''.

0 comments:

Post a Comment