
Harmonize kutoka ‘WCB’ Wasafi amesema kwa jinsi alivyolelewa na wazazi wake hapendi kabisa kuwa na skendo za wanawake.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Bado’ aliyomshirikisha Dimoand, amekiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM kuwa, akianza kuwa na skendo za wanawake wazazi wake wataanza kumfikiria vibaya.
“Unajua siku zote mimi nakataaga kuzungumzia maswala ya mahusiano kwa sababu mimi nimetoka katika familia ya kimasikini sana, halafu unavyokuja umaarufu familia yangu inatarajia kwamba itapata ridhiki kupitia mimi, so leo labda kukitapakaa taarifa kuwa Harmonize yupo na huyu, sijui yupo na huyu sidhani kama familia yangu itanielewa, wao watajua pesa nazopata kwenye muziki nazimaliza kwa wanawake,” alisema Harmonize.
Aliongeza, “Halafu mama yangu alikuwa akinisupport sana kwenye muziki wakati naanza. So akiona nipo na wanawake anaweza akakunja moyo basi huyu asifanikiwe,”
Pia Harmonize alisema video yake na Huddah ambayo ilisambaa katika mitandao ya kijamii ilikuwa ni project na aliamua kuifuta ili isije ikamletea matatizo.
0 comments:
Post a Comment