Hit maker wa ‘mkwaju’ wa Bado kutoka WCB, Harmonize, amesema kuwa mama mtoto wa Diamond Plutnumz, shemeji yake, Zari huwa hataki chakula anachotakiwa kula Diamond kipikwe na msaidizi wa kazi au mtu yeyote nyumbani.
Akizungumza na ripota wa WHarmonize amedai huwa anavutiwa sana na tabia hiyo ya kujali inayooneshwa na shemu wake.
“Yani Zari ni shemeji bora kwangu, kwanza chakula cha Diamond hakipikwi na yeyote zaidi yake, so akimuwekea na mimi huwa nakula pia sababu Diamond nae hapendi kula peke yake” Alisema.
Msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Rajabu, yupo chini ya kampuni ya kusimamia muziki ya Icon Diamond, ya Wasafi Classic Baby.
0 comments:
Post a Comment