Pam D
Binti
ambaye sasa hakamatiki kwenye ulimwengu wa muziki Bongo, Pam D
amefunguka kuwa, sasa hivi anasitisha kolabo na wasanii wa kiume akiwemo
yule aliyemtoa, Mesen Selekta akidai kuwa amegundua wanamlemaza.
Akifungukia muziki anaofanya kwa sasa, Pam D alisema, anajua anacho
kipaji na anaweza kusimama yeye kama yeye hivyo ni wakati wake sasa wa
kutoa ngoma zake kali.
“Siwezi kukataa, Mesen kanipa sapoti kubwa
sana mpaka kufikia hapa lakini sasa nimeona nisimame mimi kama mimi
nione nitafika wapi, unajua wakati mwingine ukishirikisha sana wasanii
waliokutangulia, hasa wanaume unajilemaza, kipaji chako kinashindwa
kuonekana vizuri,” alisema Pam D.
Kwa sasa mwanadada huyo anaandaa
ngoma yake mpya baada ya kufanya poa na traki zake zilizotangulia kama
vile Popolipopo na Nimempata.
0 comments:
Post a Comment