Hayo yamebainika wakati watoto 101 kati ya mia tano wakipokea msaada wa takribani Shillingi millioni 222 laki 2 kusaidia kutibu watoto katika taasisi hiyo.
Baadhi ya watoto hao ni kutoka mkoani Kilimanjaro ambapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu ametangaza kuwasaidia kuwasomesha watoto wawili mara baada ya kufanyiwa upasuaji.
Akizungumzia Idadi ya watoto wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Prof. Mohamed Janabi anasema watoto hao wanatoka katika mikoa mbalimbali nchini wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wiki ijayo ambao ni watoto 40 kati ya watoto 101 huku watoto 500 kati yao wakusubiri upasuaji mwaka huu.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka taasis hiyo, Dkt. Naiz Majani amesema Idadi ya watoto wanaozaliwa na ugonjwa wa moyo nchini ni kubwa ambapo katika kila watoto mia moja mmoja huzaliwa na magonjwa ya moyo, mwaka jana watoto 1,300 walifika katika taasis hiyo kupatiwa matibabu miongoni mwao 600 walibainika kuwa na magonjwa ya moyo na hivi sasa 450 wanasubiri kupatiwa matibabu.
Waziri wa afya, maendeleo ya jamii , jinsia wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu amesema serikali imefanya juhudi mbalimbali za kuboresha huduma za upasuaji wa moyo nchini na kuondokana na gharama za kupeleka wagonjwa wa moyo nje ya nchi.
Katika hatua nyingine waziri Ummy amesema kuwa serikali ya Tanzania inadaiwa jumla ya Shilingi Bilioni 29.7 kutokana na gharama za upasuaji wa magonjwa ya moyo kwa wagonjwa waliokuwa wanakwenda kutibiwa magonjwa ya Moyo nje ya nchi.
Mhe. Mwalimu amesema kuwa Wizara ya Afya na Serikali ya awamu ya Tano inaenzi vyema jitihada zilizofanywa na Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete za kuanzisha Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete itakayosaidia kwa sehemu kubwa kupunguza gharama za kupeleka wagonjwa wa moyo nje ya nchi.

0 comments:
Post a Comment