Wednesday, March 30, 2016

Mideast Egypt Hijacked Plane
Mwanaume aliyeelezewa kama mwenye matatizo ya akili, aliiteka ndege ya shirika la EgyptAir iliyotokea Misri kwenda Cyprus na kutishia kuilipua.


Mfanyakazi wa ndege ya EgyptAir akikumbatiwa na ndugu zake baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Cairo, Misri

Mabomu aliyokuwa nayo yamedaiwa kuwa feki na aliwaachia abiria wote baada ya kuwashikilia kwa saa sita. Mtu huyo mwenye miaka 59 anadaiwa kufanya hivyo kwasababu ya ugomvi na mke wake wa zamani.

Mtu huyo alibainika kuitwa Seif Eddin Mustafa. Baada ya ndege hiyo kutua Larnaca, mtekaji aliomba kuongea na mke wake wa zamani raia wa Cyprus aliyeletwa uwanjani hapo naye akampa barua.
Mustafa kisha aliomba kuongea na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya na miongoni mwa madai yake yalikuwa ni kuachiwa kwa wafungwa wa kike waliofungwa kwenye magereza ya Misri. Yeye na mkewe walidaiwa kuachana mwaka 1994 na walikuwa na watoto wanne.
Baada ya hapo alikamatwa na polisi wanaopambana na ugaidi.

0 comments:

Post a Comment