Umekuwa
mwaka mgumu kwa MultiChoice Africa. Masoko yetu yameathirika kutokana na
kuporomoka kwa bei ya bidhaa na mafuta na kushuka kwa thamani ya shilingi ya
kitanzania. Gharama nyingi za MultiChoice zipo katikadolayaKimarekanikituambachokilitulazimisha
kuongeza bei katika mwaka 2015.
Lakinihatupopekeyetu,wateja
wetuambaoni rasilimali yetu kuu, wanateseka. Kwa hiyo tutafanya kitu kidogo.
Tumeamua kujitwisha sehemu ya matesonahivyoHATUTAONGEZA beikwawateja wa vifurushi
vyote vya DStv kama ambavyo tumekuwa tukifanya kila mwezi Aprili. Pasipo
majanga mengine ya kiuchumi yasiyotarajiwa, hatutarajii ongezeko la bei katika
mwaka huu wa 2016.
Wateja
ndio sababu ya uwepo wetu, kwa hiyo tunadhamiria kuwaletea maudhui na vipindi
bora kabisa kwa bei nafuu. Tunataka muwe na wakati na uzoefu murua wa burudani
za hapa nyumbani na kimataifa katika televisheni.
Tuliianza
safari mwezi uliopita tulipozindua chaneli mpya za SuperSport ili kuwaletea
Ligi Kuu Ya Uingereza (EPL), Ligi Kuu ya Hispania(La Liga) na Michuano Ya
Mataifa Ya Ulaya (EURO 2016) kwa wateja wa kifurushi cha DStv Compact na
hatuishii hapo. Mwezi huu wa Aprili, chaneli za DStv zitaonyesha misimu mipya
na kisasa kabisa ya vipindi mfululizo ukiwemo msimu wa 6 unaosubiriwa kwa hamu
wa Game Of Thrones kuanzia kwenye
M-Net Edge, Express kutoka US, sambamba na telenovela mpya ya Hush ndani ya Africa Magic Showcase na The Voice: Nigeria. Wateja pia
wataburudishwa na chaguo za shoo mbalimbali za burudani za ndani na kimataifa
zinazopatikana katika vifurushi vya DStv ikiwemo telenovela mpya ndani ya Zee
World, East Meets West wakati
marathoni ya maudhui ya filamu “Wedding Season” ndani ya chaneli ya Universal
itakonga mioyo ya watazamaji kwa chaguzi kabambe za filamu za mapenzi na
vichekesho. Marathoni zaidi zinawasubiri ndani ya Studio Universal ambapo
‘Manscape’, ‘April Fools’, ‘Getting Away With it’ na marathoni za Steven
Spielberg zitawaacha na vicheko na msisimko.
Waigizaji
wa Hollywood wenye mvuto na wanaong’ara zaidi wataonyeshwa kupitia E!
Entertainment huku #Richkids Of Beverly
Hills ikirudi na onyesho la kwanza la LA
Clippers Dance Squad. Jipatie kiti cha mbele kushuhudia nyota maarufu
wanapopita katika zulia jekundu katika maonyesho yaliyosheheni nyota wa
uigizaji na burudani katika Black Girls
Rock 2016 ndani ya BET na 2016 MTV
Movie Awards ndani ya MTV Base. Mashabiki wa soka na wateja wa vifurushi
vya DStv Premium, Compact Plus na Compact pia watapatiwa burudani ya maonyesho
ya moja kwa moja kutoka mechi za Ligi
Kuu Ya Uingereza (EPL), Ligi Kuu Ya Hispania (La Liga) na michuano ya Kombe La
Mataifa ya Ulaya 2016(Euro 2016) ndani ya SS3, SS11 na SS12 huku upande wa
Hispania wakijiandaa na mechi inayosubiriwa kwa hamu ya El Classico kati ya
Barcelona na Real Madrid tarehe 3 Aprili.
KaimuMenejaMkuu,
Francis Senguji amesema, “ Tunayo furaha
kubwa kutangaza kwamba hakutokuwa na ongezeko la bei katika vifurushi vyote vya
DStv Aprili hii. Pasipo majanga mengine ya kiuchumi yasiyotarajiwa, hatutarajii
ongezeko la bei katika mwaka huu wa 2016.
Kwa maana hiyo mwezi ujao, wateja wa DStv watarajie kuendelea kupata
burudani za kuvutia kutoka DStv pasipo gharama zozote za ziada”
Kwa taarifa zaidi juu
ya vifurushi na vipindi au shoo zijazo, tafadhali tembelea www.dstv.com
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment