Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye wengi humwita Malkia wa Bongo fleva Lady Jaydee au Komando, ametoa sababu ya yeye kutomfuata (follow) mtu yeyote kwenye mitandao ya kijamii.
Akiongea kwenye kipindi cha PlanetBongo kinachorushwa na East Africa Radio, Lady Jay Dee amesema ameamua kutom-follow mtu yeyote kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo twitter na instagram, ili kuleta usawa kwa mashabiki wake.
"Kwa sababu siwezi ku-follow watu wote, kama watu labda laki tano wanani-follow alafu ni-follow back watu laki 5, ili kuondoa tu ile lawama kwa nini umem-follow fulani na kwa nini hujam-follow fulani, nikaona nifanye usawa tu kwa watu wote, na ninachokiongelea zaidi sababu mimi ni msanii watu wanafuatilia kazi, basi wafuatailie kazi zaidi",alisema Jay dee.
Pia Msanii huyo ambaye kwa sasa yupo chini na uongozi mmoja na Alikiba, ameelezea maana ya neno ambalo limebeba wimbo la Ndi Ndi Ndi, na ametoa ruhusa kwa mtu yeyote kulitumia.
"Ndi Ndi Ndi ni fleva tu kama mseme la la la, na naachia kila mtu aweze kuitumia anavyotaka kwa sababu ni mali ya umma", alisema Jay dee

0 comments:
Post a Comment