Monday, March 21, 2016


Tangu siku ya Ijumaa kumekuwa na Habari mbaya kwa upande wa Taaluma ya uandishi wa habari nchini Tanzania.
Ni kutoweka kwa ripota wa idhaa ya Kiswahili Ujerumani DW, Salma Said ambaye alitekwa na watu wasiojulikana uwanja wa Ndege JK Nyerere jijini Dar es salaam.
Sasa kamanda wa polisi wa Dar es Salaam Simon Siro, jana amethibitisha kupatikana kwa mwanahabari huyo.
Mume wa Salma Said, Bw Ali Salim Khamis,  amesema kwa sasa Salma anatoa maelezo kwa polisi Dar es Salaam.
Bado kizungumkuti kimetanda na swali zito, la wapi mwanahabari huyu aliwekwa kizuizini kwa siku tatu hizi??

0 comments:

Post a Comment