Kama unakumbuka mnamo mwaka 2012 kulitokea mgomo wa madaktari nchini Tanzania ambapo serikali ya Tanzania ilichukua uamuzi wa kuwasimamisha kazi Maafisa wa Ngazi za juu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika hatua muhimu ya kumaliza mgomo wa madaktari uliokuwa unaendelea mwaka huo.
Kutokea kwa mgomo huo wa madaktari mwaka 2012 kumemgusa Naibu waziri wa Afya,Dr.Hamisi Kingwangala ambaye kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter kaandika..’Mgomo wa madaktari haukusababisha vifo vya watu kama wachache wanavyodai sababu tulipogoma tulibakisha watoa huduma za dharura na wodini’ Hamisi Kingwangala


0 comments:
Post a Comment