Friday, March 11, 2016

Rapper wa Tanzania Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa haimpi shida kuona video yake ya Shika adabu yako haichezwi kwenye vituo vya Tv na kudai kuwepo online tu inatosha
Nay amesema video ya wimbo huo ambao ulifungiwa na BASATA licha ya kutochezwa kwenye vituo vya Tv imefika pale alipotaka kwani anaamini ndio video ya Hip Hop iliyoangaliwa zaidi kuliko zote kwa muda mfupi.
Huu wimbo BASATA waliufungia japo sikupata rasmi ndio maana nikaachia video yake Youtube tu ili nisiwaangushe mashabiki zangu,lakini inafanya poa sana,huenda ikawa video ndio video ya hip hop iliyotazamwa zaidi kwa muda mfupi na imefika matarajio yangu” alifunguka Nay wa Mitego.

0 comments:

Post a Comment