Tuesday, March 15, 2016


12509174_10153372908158379_166997376138407366_n
Ambwene Yessayah aka AY ameweka rekodi nyingi mwaka huu kupitia wimbo wake Zigo. Wimbo huu ulipotoka February 2 mwaka jana, kila mtu aliamini kuwa ni wimbo utakaofika mbali. Utamu wa melody na mdundo wake uliyafanya masikio ya wengi yashindwe kuukwepa uwezo wake wa kutengeneza uraibu (addiction).

Kwa muda mrefu AY akaanza kuahidi video yake na awali alidai kuwa ingefanyika Zanzibar na Nisher ndiye angeiongoza. Miezi 10 ilipita bila kuwepo kwa video yake na wengi walikata tamaa kuwa basi ndio nitolee.
Lakini, AY aliamua kulipa deni lake kwa kuwapa mashabiki kitu kizuri zaidi. Aliachia video ya Zigo Remix, January 21 akiwa na Diamond Platnumz. Utamu wa Zigo ulirudi upya na tena ukiwa umeongezeka maradufu. Diamond aliongeza kitu kikubwa kwenye wimbo huo ambao ulirudi tena kwenye rotation za redio.
Video yake ilianza kukusanya views kwa fujo na kutengeneza wastani wa kuangaliwa kwa zaidi ya mara laki moja kwa siku kwenye Youtube. Ndani ya siku nne, iliangaliwa kwa zaidi ya mara 450k. Audio yake nayo ikaweka rekodi nyingine kwenye mtandao wa Audiomack kwa kuwa miongoni mwa nyimbo zilizosikilizwa zaidi duniani katika wiki ya hiyo ya January 22.

Baada ya wiki moja tu, video hiyo ikawa imeangaliwa kwa zaidi ya mara milioni moja. Kila mtu anakumbuka jinsi ambavyo wimbo huu ulitrend kwenye mitandao ya kijamii kwa zaidi ya wiki mbili.

Hata hivyo, jicho la mamlaka ya mawasiliano, TCRA liliona kitu kwenye video hiyo na kuamua kuifungia isichezwe mchana. Uamuzi huo uliiweka mamlaka hiyo kwenye kiti moto, na wao wenyewe wakakiri kuwa wimbo huo unapendwa sana.
“Wimbo huu ulikuwa kwenye demand kubwa, yaani ukimwambia mtu autoe huu wimbo ni issue na umeona reaction ya watu,” alikiri meneja mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi.

Wimbo huu umeendelea kufanya vizuri hadi sasa na kuufanya kuwa wimbo pekee uliohit mfululizo katika kipindi cha miaka miwili, 2015/16.
Wiki hii, video yake imefikisha views milioni 4 katika siku 48 tangu itoke. Sio rahisi kufikisha views hizo katika muda huo. Tayari wimbo huu umeshika nafasi za juu kwenye chart za Trace Urban, Soundcity na TV zingine za nje. Wimbo huu umekuwa wimbo wa taifa Afrika Mashariki, huku Kenya ukionekana kufanya vizuri mno.
Remix hii inatufundisha nguvu tuliyonayo watanzania kimuziki kama tukiamua kuungana pamoja na kutengeneza muziki. Kwamba hits kama hizi zinaweza kutokea na sio lazima kumshirikisha msanii mkubwa wa nje ya Tanzania. Inatufundisha kuwa wasanii hawapaswi kuzipuuzia hits zao wanazofanya.
Kwamba zinaweza zikadumu zaidi pale ambapo watazifanyia remix kwa kuongeza ladha na nguvu kutoka kwa wasanii wengine. Hawapaswi kuogopa kwamba wakiwashirikisha wasanii wengine kwenye remix wanaweza kufunikwa, bali watambue kuwa kumwalika msanii mwingine kwenye hit yako, ni kuipa nguvu zaidi ngoma na kuiongezea muda wa kuishi.

CHANZO na Bongo5.

0 comments:

Post a Comment