Sunday, March 27, 2016

Taarifa kutokea Mwanza 88.1, ni hii ya Majambazi kuvamia maduka eneo la Bugarika kata ya Pamba Nyamagana wakapora pesa na kuuwa watu wawili kwa risasi na wengine saba kujeruhiwa usiku wa wa tarehe 25, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa MwanzaJustus Kamugisha   mbele ya  waandishi wa Habari kayasema haya…
Image00002
Tarehe 25 majira ya saa 08:06 usiku, mtaa wa Bugarika sokoni wilaya ya Nyamagana Mwanza, majambazi walionekana wakiwa watatu wakiwa na silaha aina za SMG au SARwalivamia duka la mfanya biashara wa bidhaa na M Pesa Daniel Marwa, walifyatua risasi na kupora fedha kiasi cha Mil.2 na vocha za mitandao thamani ya Laki 8; – RPC Justus Kamugisha
Image00001
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mwanza, Justus Kamugisha
Hao majambazi waliweza kuwapiga risasi watu wa wawili na kupoteza maisha na wengine saba wamejeruhiwa, waliopoteza maisha ni Julius Wankaba (30), dereva bodaboda na Mama Yuni mmiliki wa duka la vipodozi, majeruhi watano wapo Bungandona wawili wapo Hospitali ya Mkoa ya Sekouture kwa matibabu;-RPC Kamugisha
Image00004
Kwa yule atakaeweza kushirikiana na Jeshi la Polisi na kufanikiwa kuwa kamata majambazi, Jeshi la Polisi litatoa zawadi ya pesa kiasi cha sh.millioni moja kwa ajili ya kusaidia hilo;- RPC Justuc Kamugisha.
Bonyeza Play kusikiliza

0 comments:

Post a Comment