Saturday, March 26, 2016

jacob-zuma-drum
Siku ya Ijumaa ofisi ya Urais Afrika Kusini ilifahamisha kuwa rais Zuma atasafiri kwenda Saudi Arabia katika ziara ya kikazi itakayosaidia kukuza uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Rais Zuma atasafiri kwenda Saudi Arabia siku ya Jumapili ingawa ziara yake ya kikazi katika falme za kiarabu itaanza rasmi siku ya Jumatatu.

Aidha ziara ya Jacob Zuma Saudi Arabia itaimarisha mahusiano ya kiuchumi na kisiasa baina ya nchi hizo mbili.

Zaira hiyo itakuwa ziara ya tatu urais nchini Saudi Arabia ya kwanza ilikuwa ni ya marehemu rais Nelson Mandela mwaka 1997 na pili ilikuwa ya rais wa zamani Thabo Mbeki mwaka 2007.

0 comments:

Post a Comment