Posted by Williammalecela.com on Saturday, March 26, 2016

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Bwana Said Hassan Said, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyeikiti wa Baraza la Mapinduzi alimteua Bwana Said Hassan jana kushika wadhifa huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 55 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Hafla ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu huyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment