Rapa mahiri nchini maarufu kama Roma Mkatoliki amesema wimbo wa Nay wa Mitego wa Shika Adabu Yako unashtua kutokana na mambo yalizungumzwa ndani yake ambayo pia siyo mapya ni yaleyale tu.
Roma ameeleza hayo alipokuwa akijibu swali katika mahojiano yake na kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Afrika Radio, swali lililomtaka kutoa maoni yake kuhusu kufungiwa kwa wimbo huo wa Nay kama ulivyofungiwa ule wa kwake wa Viva Roma Viva aliouachia Septemba 9 mwaka jana.

Roma amesema kiukweli wimbo ule unashtua ukiusikiliza lakini ungekuwa wake pia angepigana usifungiwe kwasababu ulipokewa vizuri na mashabiki, hivyo ulitakiwa kufanyiwa marekebisho kwa sehemu zilizoonekana hazina maadili lakini siyo kuufungia moja kwa moja.
0 comments:
Post a Comment