
Siku
tatu baada ya kuibuka kwa kashfa ya rushwa miongoni mwa wajumbe wa
Kamati za Kudumu za Bunge, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru) imemuita Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kumhoji.
Muda
mfupi baada ya taarifa za kashfa hiyo kuwa wazi, Zitto na mwenzake wa
Nzega Mjini, Hussein Bashe ambao ni wajumbe wa Kamati ya Huduma za
Jamii, walimuandikia barua Spika wa Bunge, Job Ndugai kujiondoa kwenye
nafasi zao ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.
Zitto
alithibitisha kupata wito kutoka makao makuu ya Takukuru ili kuhojiwa
juu ya sakata hilo na akapongeza kuwa endapo vyombo vya Serikali
vitakuwa makini kushughulikia tuhuma zote zinazoelekezwa kwa wanasiasa
na watumishi wengine wa umma, itasaidia kuongeza uwajibikaji na
kupunguza uzushi kwa wananchi.
“Nimepata wito huo kupitia Ofisi ya Bunge. Nasikia Bashe ameitwa pia. Nafurahi wito wetu wa uchunguzi umechukuliwa kwa uzito unaostahili na tutatoa ushirikiano wote kwa vyombo vya uchunguzi ili kumaliza zoezi hili kwa haraka na kwa ufanisi,” alisema Zitto.
0 comments:
Post a Comment