Dubai imepiga marufuku wanawake waja wazito kuvuta ama hata kuingia katika migahawa inayouza Shisha .
Hatua hiyo inafuatia shinikizo la kuimarisha afya ya umma na haswa afya ya mama waja wazito.
Sheria hiyo inawadia baada ya kampeini ya kuwazuia wanawake wajawazito kuingia pahala panapovutiwa sigara jarida la aGulf News linasema.
Kampeini hiyo inayoendeshwa kwa kutumia mabango na picha ya mwanamke mjamzito akiambiwa na mwanaye aliyeko tumboni kuwa ''Uamuzi wa kuvata au la ni wako,,,sio wangu''
Mabango hayo yanaeleza kuwa watoto ambao hawajahitimu miaka 18 na wanawake wajawazito hawaruhusiwi kuvuta shisha au sigara.
"Kauli hiyo ni ya serikali wala sio hoja ya kujadiliwa na yeyote '' alisema mkurugenzi wa afya ya umma wa Dubai bwana Marwan Al Mohammed.

0 comments:
Post a Comment