Mshindi wa tuzo ya AMVCA 2016, Elizabeth ‘Lulu’ Michael kupitia filamu yake ya Mapenzi alikutana na Sammisago kupitia kipindi cha Friday Nite Live na kujibu swali kuhusu mahusiano yake na CEO wa EFM na Dj maarufu Tanzania Dj Majay.
Lulu anasema “Ninaweza nikasema ndio wakati sio kweli na ninaweza kusema hapana wakati ni kweli, lakini kikubwa zaidi kimaadili ya kitanzania, kimaadili niliyofundishwa mimi, mchumba hatangazwi, ndoa ndiyo inatangazwa ila Sam,kama ni kweli ndoa itakuja na watu wataona, lakini siwezi kutangaza wakati bado hatuna mikakati ya ndani zaidi”.
0 comments:
Post a Comment