Friday, March 4, 2016


Msanii Stamina amesema hatua ya wasanii wa muziki Hip Hop nchini kwenda kushoot video nje inaongeza ushandani wa kibiashara.

Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Stamina amesema na yeye yupo njiani kuelekea huko kama alipata kazi sahihi ya kumpeleka.

“Mimi sitaki nijipeleke Afrika Kusini kushoot video, mimi nataka video ndio inipeleke Afrika Kusini kushoot video,” alisema 
“Muziki unakuwa na biashara inatanuka, lakini sio kila video ni lazima ushoot nje ya nchi, kwa mfano mimi nachokitaka kipo hapa hapa Tanzania na kinahitaji mazingira ya Tanzania, sidhani kama nikienda Afrika Kusini nitakuwa nimeitendea haki video yangu. Ni bora uwalete director hapa nyumbani, lakini ukitaka kujua kuna gharama kiasi gani hebu angalia wasanii wangapi wameweza kuwatoa madirector South na kuwaleta hapa, ni Diamond peke yake. Lakini wengine wote wanaenda kushoot huko huko, kama kweli wanatafuta ubora wa kazi kwa nini wasiwalete hapa. Kwa hiyo unaweza kuona kuna gharama kubwa zakuwaleta hapa. Kwa hiyo mimi naangalia ubora kwa sababu hata video za hapa nyumbani siku hizi zinachezwa kwenye TV za kimataifa,”

Mwana FA pamoja na Fid Q ni miongoni mwa wasanii wapya wa Hip Hop ambao wameanza kushoot video zao na director wa kubwa wa nje. AY ndiye msanii wa Hip Hop ambaye alikuwa anashoot video nje mara kwa mara.

0 comments:

Post a Comment