TAASISI ya Wanawake Ndani ya Jamii (Woiso) ambayo ni taasisi isiyokuwa ya kiserikali inayotoa elimu kwa jamii hususani kwa wanawake na watoto, imekuja na kipindi cha watoto kijulikanacho kama “Thamani Yetu Watoto” kitakachokuwa kikiruka hewani kupitia televisheni ya Star TV kuanzia Jumamosi Machi 5 mwaka huu saa 3:30 usiku na kurudiwa Jumapili saa 12:30 jioni.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, mwanzilishi wa kipindi hicho, Janeth Mwasawala, amesema taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 2013 chini ya Wizara ya Maendeleo ya jamii, Wanawake, Wazee na Watoto kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na maisha, kujitambua na afya na mazingira.
Mwasawala amesema kipindi hicho kitatoa elimu kwa makundi muhimu kwa jamii ili kuijenga jamii yenye weledi na kujitambua na fursa ya watoto kuongea na kutoa maoni yao kuhusu mambo wanayoyapenda, changamoto wanazokumbana nazo katika maisha yao ya kila siku wakiwa nyumbani na hata shuleni .
Aidha alifafanua kuwa kupitia kipindi hicho watawaeleza watoto mambo wanayopaswa kutendewa au kutenda pamoja na kueleza vipaji na ndoto zao, jambo litakalosaidia kujenga jamii yenye maadili na maendeleo kwa maslahi ya taifa.



0 comments:
Post a Comment