Familia ni kitu cha kwanza kwa Diamond kwa sasa. Actually familia inapaswa kuwa kitu cha kwanza kwa kila mtu, nikiwemo mimi. Watu wake muhimu kwenye maisha yake ni mwanae, Tiffah, mpenzi wake Zari the Bosslady na mama yake, Sandra.
Wakati akiendelea na ziara yake ya Ulaya, aliyoipa jina, From Tandale to The World Tour, hitmaker huyo ameona ni vyema kuichukua familia yake na kuzunguka nayo.
Anazunguka na timu kubwa. Ukiitoa familia yake of course bila kumsahau binamu yake, Romy Jones, Diamond ameenda Ulaya akiwa na dancers wake wanne, mpiga picha, meneja (wanapokezana Sallam na Babutale na watu wengine takriban wawili akiwemo mke wa Tale.
Ni msafara mkubwa ambao sehemu yake bila shaka haupo kwenye bili anazotakiwa kugharamikia promota wa show husika. Kimsingi inaonekana wazi kuwa Diamond anatumia muda huo pia kama vacation ya kufurahia na familia yake. Hiyo inamaanisha kuwa anatumia gharama kubwa katika ziara hiyo.
Hata hivyo kwa fedha anazoingiza kutoka kwenye vyanzo lukuki, gharama hizi ni kama tone kwenye ndoo ya maji. Mtandao wa Global Publishers umedai kuwa ziara hiyo huenda imemgharimu takriban shilingi milioni 100. Makadirio hayo yanaweza kuwa makubwa sana lakini ukweli ni kwamba anatumia gharama kubwa na ni ziara ya kifahari.
“Diamond ameandaa mkwanja usiopungua milioni 100 kwa ajili ya msafara wake. Fedha hizo zitatumika kuanzia usafiri wa ndege kwenda na kurudi, chakula, shopping na malazi kwa kipindi chote cha wiki tatu atakachokuwa Ulaya,” mtandao huo umekinukuu chanzo kimoja.
GPL wamedai kuongea na msanii huyo kumuuliza kama gharama hizo zimefika.
“Siwezi kusema moja kwa moja kama inafika au la lakini inaweza kufika na hata zaidi. Wewe chukulia mimi tu na familia yangu (yeye, Tiffah, Zari na ndugu zake) nimetenga kama dola 30,000 kwa ajili ya usafiri, malazi na shopping za hapa na pale sasa vipi kuhusu timu nzima ya madansa, meneja na wengine?” wamemnukuu Diamond.
Kwa vyovyote vile huu ni wakati wake kula matunda ya jasho lake na kama unaweza kuweka tabasamu kwenye sura za unaowapenda, hakuna jambo jingine kubwa zaidi ya hilo.

0 comments:
Post a Comment