Monday, March 28, 2016


tiny-tip
Rapper T.I. hataki mchezo.. Yeye na mke wake, Tiny wamepata mtoto wao wa tatu, wa saba kwa rapper huyo.

Mtoto huyo wa kike alizaliwa wiki iliyopita. Taarifa hiyo ilitolewa na mtoto wa dada yake na T.I., Kamaya Harris.

“My little cousin is here. Last night I went to go see my auntie and she had the baby today,” alisema kwenye Snapchat.
Tayari familia hiyo ina watoto sita wengine, Messiah, Domani, Deyjah, King, Major na Zonnique.

Watoto wake wa mahusiano yaliyopita ni wa kiume wawili aliozaa na Lashon Dixon: Messiah Ya’Majesty Harris na Domani Uriah Harris. Ana mtoto wa kike Deyjah Imani Harris aliyezaa na msanii wa R&B, Ms. Niko.

Pia kwenye ndoa yake na Tiny, T.I. ana watoto wa kambo, Zonnique Jailee Pullins na Zonnie Zebo Pullins.

0 comments:

Post a Comment