Kutokana na kushiriki katika mashindano matatu kwa wakati mmoja,
klabu ya Yanga inakabiliwa na ratiba ngumu ya kucheza mechi nne ndani ya
siku kumi.
Wakati Simba ikiendelea kujikita kileleni wenzao Yanga na Azam ratiba
imeendelea kuwa ngumu kwao kutokana na mrundikano wa mechi za viporo na
zile za kimataifa. Bodi ya ligi kuu nchini Tanzania (TPLB) imetoa mabadiliko ya ratiba
ya ligi kuu Tanzania Bara , kwa mujibu wa ratiba hiyo Yanga itacheza
Ijumaa, Jumapili na Jumatano kabla ya Kuwavaa ‘Waarabu’ Al Ahly siku ya
Jumamosi tarehe 9 Aprili.
Yanga wanatarajia kushuka dimbani siku ya Ijumaa ya tarehe 1 kuwavaa
Ndanda katika kombe la Azam shirikisho, na siku mbili mbele watashuka
tena dimbani katika uwanja wa taifa kuwakabili Kagera Sugar siku
jumapili tarehe 3 Aprili. Baada ya hapo Yanga Itapumzika siku mbili na siku ya tatu watakutana na
Mtibwa Sugar, katika mchezo unaotarajiwa kutimua vumbi tarehe 6 Aprili
kunako dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Upana na ukubwa wa kikosi cha Yanga utapimwa zaidi wakati watakopkuwa
na siku mbili tu za kupumzika kabla ya kuwavaa Al Ahly katika mchezo wa
hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika siku ya Jumamosi ya tarehe 9
Aprili.
0 comments:
Post a Comment