MBUNGE wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Vicky Kamata (Viti maalum CCM) amesema kwambaamejisikia furaha na ana kila sababu ya kuiomba kampuni ya Msama Promorions kutimiza ahadi yake ya kulipeleka Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Alisema kuwa mbali na burudani naamini kuwa hata wananchi watanufaika na Tamasha hilo kwa ujumbe kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kuhusiana na mauaji ya walemavu wa ngozi 'albino' pamoja na vikongwe.
Kwa kweli mauaji hayo yanatokana na imani ya kishirikina lakini kwa tamasha hili ambalo ni sawa na kutangaza injili kwa njia ya nyimbo itaweza kuvunja nguvu za kishetani na wananchi kumrudia mungu.
“Nimefurahishwa katika hili naamini nguvu ya mungu itaenda kutenda kazi yake hivyo ni imani yangu kuwa watu watabarikiwa kwa kuvunja nguvu ya shetani na watu kumrudia mungu ,” alisema Mbunge huyo ambaye pia ni msanii.
Aidha Mbunge huyo alisema angefurahi kama waimbaji ambao wametajwa katika tamasha hilo kama Rose Muhando, Bonny Mwaitege na Upendo Nkone wafike Geita na wamewaandalia mapokezi ya aina yake kwani wana idadi kubwa ya mashabiki.

0 comments:
Post a Comment