Tuesday, March 8, 2016


Kocha wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane baada ya weekend hii Cristiano Ronaldo kufunga goli nne peke yake katika ushindi wa goli 7-1 dhidi ya klabu ya Celta Vigo, Zidane goli hizo alizofunga Ronaldo hakuzichukulia poa.

Zidane ambaye alichukua nafasi ya Raphael Benitez, amezungumza na kusisitiza kwa mara nyingine tena kuwa Real Madrid wanahitaji kuendelea kumbakiza kikosini Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa akihusishwa kutaka kuhama.

Ronaldo baada ya kufunga goli nne peke yake dhidi ya Celta Vigo, anakuwa mchezaji wa kwanza Ulaya kufunga jumla ya goli 350 akiwa na klabu moja kwa muda mfupi.

0 comments:

Post a Comment