Posted by Williammalecela.com on Friday, April 22, 2016
 |
April 01 2016 Serikali iliwapandisha kizimbani kamishna wa zamani wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ Harry Kitilya, mshindi wa taji la Miss
Tanzania 1996 ambaye pia alikuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanibic
tawi la Tanzania Shose Sinare na Sioi Solomoni kwa tuhuma mbalimbali
zikiwemo za kula njama kutenda kosa pamoja na kosa la kughushi na
kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Kesi hiyo ilipangwa kuendelea tena leo April 22 2016 katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ambapo imeahirishwa na Hakimu
Mkazi Emillius Mchauru kwa sababu hakimu hajakamilisha uandikaji wa
uamuzi wa kuondoa shitaka la utakatishaji fedha linalowakabili
washtakiwa wote watatu. Kesi hiyo itaendelea tena April 27 2016 na
watuhumiwa wamerudishwa rumande.
|
0 comments:
Post a Comment