Magufuli amtumbua Mnikulu
RAIS Dk. John Magufuli, amefanya mabadiliko mengine Ikulu jijini Dar es Salaam kwa kumwondoa aliyekuwa Mnikulu, Jumaa Bwando.
Vyanzo
vya habari kutoka Ofisi ya Rais vimesema Bwando, aliondolewa katika
wadhifa huo Machi 14, 2015, ambapo kwa sasa nafasi hiyo inakaimiwa na
mmoja wa maofisa wa juu wa Ikulu.
Julai
10 mwaka jana, Bwando aliteuliwa kushika wadhifa huo na Rais (mstaafu)
Jakaya Kikwete, kuchukua nafasi ya Shaban Gurumo, aliyeng’olewa baada ya
kukiuka sheria ya maadili ya viongozi wa umma inayokataza kiongozi wa
serikali kupokea zawadi zaidi ya zawadi ndogondogo na ukarimu wa
kawaida.
Kazi
ya Mnikulu ni kusimamia majengo yote ya Ikulu kwa maana ya shughuli za
utawala. Yeye ndiye anayehusika na usafi, samani na mapambo yote katika
ofisi hiyo kuu ya nchi.
Ni
mtu anayeweza kuamua mwonekano wa Ikulu uonekanaje, hata kupanga na
kuamua aina ya nguo, mashuka, mapazia yanayopaswa kutumiwa na Rais. Kwa
majukumu husika anapaswa amjue vizuri Rais.
Hatua hiyo ya Rais Magufuli ni mwendelezo wa mabadiliko aliyoanza kuyafanya Ikulu siku chache baada ya kuingia madarakani.
Hatua hiyo ya Rais Magufuli ni mwendelezo wa mabadiliko aliyoanza kuyafanya Ikulu siku chache baada ya kuingia madarakani.
Tayari
amezifumua na kuziunda upya baadhi ya ofisi za Ikulu ya Magogoni, Dar
es Salaam pamoja na kuwaondoa baadhi ya watumishi ambao hawana ulazima
katika mfumo wa utumishi wa Ikulu.
Rais Magufuli alianza kufanya ukaguzi wa ofisi moja baada ya nyingine zilizopo Ikulu, huku akitaka maelezo ya kina kuhusu shughuli zake na aina ya watendaji waliopo.
Rais Magufuli alianza kufanya ukaguzi wa ofisi moja baada ya nyingine zilizopo Ikulu, huku akitaka maelezo ya kina kuhusu shughuli zake na aina ya watendaji waliopo.
Katika
ukaguzi huo, Rais Magufuli aliamuru kufungwa mara moja kwa baadhi ya
ofisi alizobaini kuwa hazina tija na kwamba zina watumishi ambao ni
mizigo.
Baadhi ya ofisi zinazodaiwa kufungwa ni pamoja na iliyokuwa ikishughulikia chakula cha Rais na ile iliyokuwa ikijihusisha na kupokea wageni binafsi wa Rais.
Baadhi ya ofisi zinazodaiwa kufungwa ni pamoja na iliyokuwa ikishughulikia chakula cha Rais na ile iliyokuwa ikijihusisha na kupokea wageni binafsi wa Rais.
Wakati
akifanya mabadiliko hayo, Ofisa mmoja wa Ikulu alinukuliwa akisema.
“Rais Magufuli alipoingia tu Ikulu alifanya ziara ya kukagua ofisi zote
zilizopo Ikulu, alitaka kujua utendaji kazi wa ofisi hizo, lakini
alipofika kwenye kitengo maalumu cha lishe ya Rais, alisema haoni
umuhimu wa kuwepo kwa ofisi hiyo kwa sababu suala la lishe yake siku
zote linasimamiwa na mkewe Janeth.
“Akaamuru
ifungwe na watumishi wake warejeshwe walikotoka. Ofisi nyingine
aliyoamuru ifungwe ni kupokea wageni binafsi wa Rais. Alisema haoni tija
ya kuwepo kwa ofisi hiyo kwa sababu mgeni anatakiwa kufika Ikulu baada
ya kutoa taarifa, nayo aliamuru ifungwe,” alisema ofisa huyo.
Taarifa
zilisema aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Lishe Ikulu alirudishwa katika
ajira yake ya awali Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, huku watumishi
wengine wakipelekwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma.

0 comments:
Post a Comment