Moto
umeteketeza bweni la wasichana la Shule ya Sekondari ya Issenye na
kusababisha hasara ya zaidi ya Sh80 milioni na wanafunzi 43 kukosa
malazi.
Tukio hilo,
ambalo limeibua taharuki kubwa, lilitokea jana (Aprili 20) kati ya saa
5:00 na saa 6:00 mchana, ikiwa ni takriban miezi nane tangu wanafunzi
wachome duka la shule hiyo julai mwaka jana wakipinga vitendo vya
kunyanyaswa.
Mkuu wa shule
hiyo, Joseph Nyamgonja aliiambia Mwananchi kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa
kwa kuwa wanafunzi walikuwa darasani, lakini vitu vyote vya wanafunzi
vimeteketea.
Alisema bado hawajajua chanzo cha moto kuibuka kwenye bweni hilo ambalo halina umeme.
"Nikiwa ofisini niliona wanafunzi wanakimbia kuelekea bwenini. Kutoka nje niliona moshi mkubwa kwenye bweni," alisema.
"Tulifanikiwa
kubomoa mlango na kuokoa magodoro machache. Tulijitahidi kuzima kwa maji
na mchanga, lakini hatukufanikiwa baada ya paa lote kushika moto,"
alisema.
Alisema
vitanda 52 , magodoro na vitu vyote vya wanafunzi vimeteketea na
tathimini ya awali inaonyesha kuwa moto huo umesababisha hasara ya zaidi
ya Sh80 milioni.

0 comments:
Post a Comment