Tuesday, April 12, 2016

IMG-20160411-WA0001
Msanii wa muziki Dudu Baya amefunguka kwa kusema kuwa ‘majangili wa muziki’ wamesabisha wasanii wengi washindwe kufanikiwa na wachache ambao wanawamiliki kuendelea kulishilia soko la muziki.

Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Dudu Baya amesema hali hiyo imesababisha soko la muziki kushikiliwa na wasanii wachache.
“Unajua hakuna kitu kinaniumiza kichwa kama muziki kushikiliwa na wasanii wachache au mmoja,” alisema Dudu.
Aliongeza, “Kama tunataka tusonge mbele tuanze na hawa ‘majangili’ kwa sababu wao ndio chanzo cha haya yote. Haiwezekani muziki ushikiliwe na watu wachache wakati kuna wasanii wengi wako vizuri sana, lakini hawafanyi vizuri na ngoma zao hata zikawa kali hazipati airtime yakutosha”,
Dudu Baya amezitaka media kuhakikisha wanapiga nyimbo nzuri bila kuangalia niya nani ili kuokoa muziki wa Tanzania ambao kwa sasa amedai unamilikiwa na wasanii wachache.

CHANZO na Bongo5

0 comments:

Post a Comment