V
ideo Queen na Mtangazaji wa Runinga, Gifty Stanford ‘Gigy Money’
juzikati alifakamia pombe kali na kujikuta akilewa tilalila hadi
kuzimika ndani ya klabu moja iliyopo kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar.
inti
huyo asiyeishiwa na vituko alinaswa na mapaparazi wetu akiwa kwenye
hali hiyo Jumatatu liyopita (Jumatatu ya Pasaka) ambapo awali alionekana
akinywa pombe kali huku akivuta sigara. Baada ya kupombeka kwa muda
mrefu huku akionekana kama aliyekuwa na mawazo mengi, taratibu mdada
huyo aliyejaaliwa shepu alianza kupoteza ‘netiweki’.
Haikuchukua
muda refu akawa amezimika na kuwaacha watu waliokuwa wakimuangalia
wakimjadili kwa namna ambavyo alikuwa hajitambui. “Huyu bwana pombe
zitamuua, mwenyewe huwa anasema anakunywa kidogo tu, sasa mbona leo hadi
kazima, asipoangalia wahuni watamfanyizia,” alisema kijana mmoja
aliyekuwa eneo la tukio.
Baada
ya muda mfupi, alifika dada mmoja aliyeonekana kujuana na Gigy
(inaonekana alipigiwa simu) ambapo alimchukua kwa kumkokota kisha
akampakiza kwenye Bajaj wakaondoka.
Siku
moja baada ya tukio hilo, Ijumaa lilimpigia simu Gigy Money na
kumuuliza kulikoni amekuwa na tabia ya kulewa hadi kuzimika
alipopatikana alijibu: “Ni maisha yangu, haina haja kunifuatilia.”
0 comments:
Post a Comment