Saturday, April 16, 2016

Bw.Said Hamad Lugumi mmiliki wa kampuni ya Lugumi Enterprises inayotuhumiwa kupewa zabuni kwa upendeleo na Jeshi la Polisi ya Bilioni 37, ametoroka nchini ikiwa ni siku chache tu baada ya Jeshi la Polisi kuhojiwa na Kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma (PAC) juu ya kashfa hiyo iliyoligharimu taifa mabilioni ya fedha.


Katika kashfa hiyo Kampuni ya Lugumi Entesrprises inadaiwa kupewa mkataba na Jeshi la Polisi wa kufunga mitambo ya "Biometric Access" kwa ajili ya Finger Print ktk vituo 108 nchi nzima lakini mpaka sasa imefunga mitambo hiyo ktk vituo 14 tu wakati imeshalipwa Bilioni 34 sawa na 99% ya pesa yote aliyotakiwa kulipwa ambayo ni Shilingi Bilioni 37.
Kamati ya Bunge inahoji mambo makubwa matatu:
‪#‎MOSI‬
 

Ni kwanini kampuni ya Lugumi ilipewa zabuni hiyo wakati haikuwa na uwezo wala uzoefu wa kufanya kazi hiyo?. Zipo kampuni nyingi zenye uwezo na uzoefu na zilituma maombi ya zabuni lakini zikanyimwa na "tender" hiyo ikapewa kampuni ya Lugumi isiyo na uwezo wala uzoefu.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa kampuni ya Lugumi imesajiliwa kama kampuni ya uchapishaji (Printing &Publishing company) ikiwa na ofisi zake katika jengo la ATCL jijini Dar. Haijasajiliwa kama "Biometric Access Company" na haijawahi kufanya kazi zozote zinazohusiana na Biometric Access Control.

Kwa lugha rahisi ni kwamba kampuni ya Lugumi ni kama zile "stationeries" pale Mabibo Hostel zinazoprint na kutoa copy madesa ya wanafunzi lakini imepewa kazi ya kufunga mashine za "Finger Print" ktk vituo vikuu vya Polisi nchi nzima. Kamati ya Bunge inahoji ilikuaje kampuni hii ikapewa zabuni hiyo wakati haina uzoefu wala uwezo wa kufanya kazi hiyo??
‪#‎PILI‬
Kamati ya Bunge inahoji ilikuaje kampuni ya Lugumi ikapewa fedha zote za utekelezaji wa zabuni kinyume na Sheria na mkataba wa zabuni hiyo.? Kwa mujibu wa taarifa ya PAC, Mkataba unaeleza kuwa kampuni hiyo ilipaswa kulipwa asilimia kadhaa mwanzoni mwa zabuni na malipo mengine yamaliziwe mwishoni baada ya kumaliza kazi. Lakini kampuni hiyo ilikomba Bilioni 34 kati ya Bilioni 37 alizotakiwa kulipwa.



#‎TATU‬
Mkataba wa Lugumi ulisainiwa mwaka 2011 na ilitakiwa kumaliza kazi hiyo ndani ya miaka mitatu yani 2014. Lakini hadi sasa zaidi ya miaka mitano hawajaweza kufanya hata robo ya kazi waliyopewa. Mashine 14 kati ya 108 walizopaswa kufunga ni sawa na asilimia 12% tu ya utekelezaji wa zabuni. Sasa kama kampuni inatekeleza mradi kwa 12% tu ndani ya miaka mitano, je itawatumia muda gani kutekeleza kwa 100%??

NB:
Taarifa zilizotolewa na mtandao wa
https://lugumi.wordpress.com/author/lugumi/ zinaonesha kuwa Bw.Said Lugumi amemuoa mtoto wa Said Mwema aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Pia taarifa hiyo inaeleza kuwa Kampuni ya Lugumi Enterprises inamilikiwa kwa ubiya kati ya Bw.Said Lugumi
Taarifa hiyo inazidi kueleza kuwa kiwango cha elimu ya Bw.Said Lugumi ni shule ya msingi (darasa la saba) na hana uzoefu wowote wa kazi zinazohusiana na "Biometric Access". Alizaliwa mwaka 1972 mkoani Mwanza na kabla ya kuhamia jijini Dar alikuwa fundi viatu (Shoe Shiner) barabara ya Kenyatta jijini Mwanza.

0 comments:

Post a Comment