Monday, April 25, 2016

Leo nataka nikutie moyo rafiki yangu uliyevunjika moyo yes wewe unayedhani umeshindwa umekata tamaa mwenye changamoto ambayo unadhani huwezi kusimama tena
....Inuka ukiwa na sababu why unataka kusimama utashinda haijalishi upo kwe hali gani kushinda ni Lazima

Tarehe 11 February mwaka 1990 katika jiji la Tokyo, Japan kulitokea tukio ambalo lilijenga historia duniani. Hii ilitokana na pambano kubwa la masumbwi lililofanyika kati ya Mike Tyson na Buster Douglas. Wakati pambano hili linafanyika Tyson alikuwa ni bondia wa kuogopwa na wa kutisha ambaye alikuwa akishinda kwa KO katika kila pambano lake lililopita, hivyo kila mtu hakuwa na shaka kuwa Tyson angeibuka mshindi kabla raundi tatu hazijamalizika kama iilvyokuwa kawaida yake.

Mara baada ya kuanza pambano kama kawaida Tyson alitumia uwezo wake na nguvu zake kumshambulia adui yake kwa nguvu na kwa masumbwi makali akitarajia kumuangusha na kumshinda katika raundi za mwanzo. Cha kushangaza hadi raundi ya nane inafika mpinzani wake alikuwa bado amevumilia na bado anaendelea kupigana. Ilipofika raundi ya 8 Tyson alimpiga ngumi ya katafunua (Uppercut) mpinzani wake na alianguka kwa anguko ambalo hakuna mtu alitarajia atainuka tena.

Lakini wakati Tyson anaanza kufurahia kuwa ameshinda, akashangaa Buster Douglas anainuka na akaja na nguvu mpya na ilipofika raundi ya 10 akamshinda Tyson kwa KO na kuweka historia kuliko matarajio ya watu wengi. Miaka 25 baadaye, Douglas alihojiwa na kuulizwa ni nini kilimfanya ashinde pambano lile, majibu yake yanatoa funzo kubwa sana.

Anasema wakati amesaini kupigana na Tyson mama yake alikuwa anaumwa sana na kabla tu ya pambano alifariki na kabla hajafariki alimwambia kuwa zawadi kubwa anayoweza kumpa ni kumshinda Tyson. Lakini pia, kipindi anaenda kupigana na Tyson alikuwa ametoka kuachana na mke wake wa ndoa. Lakini pia maisha yake ya kifedha yalikuwa yameyumba. Alikua na hali ngumu sana kiuchumi, hivyo kumshinda Tyson ilikuwa ni fursa muhimu kwake kubadilisha maisha yake kiuchumi.

Hivyo ushindi wake ulianzia kwenye “SABABU” hizi. Douglas anasema ili ufanikiwe hata pale watu wanapofikiri hauwezi kufanikiwa, kitu cha kwanza ni kuwa na sababu(why) yenye nguvu kuliko kuanza kuwaza utafanikiwa kwa namna gani(How). Ili mradi sababu yako(Why) ina nguvu basi namna(How) lazima itapatikana.
Lakini pia wakati ameanguka chini na akaona kuwa kama ameishiwa nguvu kabisa za kuinuka tena, maswali mengi yalipita ndani yake. Je,niendelee? Lakini mbona nimeishiwa nguvu? Hata hivvyo nimejitahidi nimepigana hadi raundi hii nikiacha hapa nimefanikiwa pia n.k

Lakini mara baada ya kukumbuka sababu yake (why) akaamua kuamka kuendelea bila kujali atashindaje (how).
Douglas anasema mara baada ya kuamka aliona macho ya Tyson yakikata tamaa kwani hakuamini kama anaweza kuinuka tena; na kwa maelezo yake anasema hapo ndipo alipomshinda Tyson. Alimpiga mfululizo na kufika raundi ya 10 Tyson akaishiwa nguvu hivyo akamshinda kwa Knock Out (KO).

FUNZO;
 

Kwenye maisha huwa tunapita katika majira kama haya ambapo inaonekana kama matatizo yanayotukabili ni mazito kuliko tunavyoweza kuyashinda, matokeo yake tunakata tamaa kwani kila mtu anatuambia hatutaweza. Lakini tusichojua ni kuwa kama tutapata sababu nzito inayotusukuma kuziishi ndoto zetu, hatutajali changamoto zinazotukabili. Tutapambana na tutashinda.
Je,una sababu nzito (why) inayokusukuma kuiishi ndoto yako?Kumbuka uzito wa SABABU yako ndio itajulisha kama utafanikiwa ama lah.

Tunapokuwa tumeanguka chini kiuchumi, kibiashara, kimahusiano, kielimu tunaona kama vile hatuwezi kuinuka tena. Kuna maswali mengi yanapita katika katika akili yetu. Hivi nitaweza kuinuka tena? Si bora niache tu, nimejaribu kila namna imeshindikana, labda sitaweza kuinuka tena, maana nimeishiwa nguvu na kila mtu anajua hilo.Tusichojua ni kuwa kama ilivyokuwa kwa Douglas. Mara tutakapoamua kuinuka wakati bado maumivu ni makali na hali inoenekana imeshindika, ndivyo Tyson wetu atakavyokata tamaa na tutamshinda.

KUMBUKA: Ushindi wako uko kwenye uwezo wako wa kuinuka na kuendelea pale ambapo kila mtu anaona kwamba hautaweza kuinuka na kufanikiwa tena. Leo usikubali kuogopa kumkabili Tyson wako. Usikubali Kubakia chini baada ya kuangushwa na changamoto zako. Hata kama bado maumivu unayasikia, bado nguvu hazijarudi, Inuka na uanze upya kuifukuzia ndoto Yako na utashinda. Inawezekana. Ndoto Yako Inawezekana.

0 comments:

Post a Comment