
WATU
wapatao nane wameripotiwa kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa
baada ya jengo la ghorofa sita lililoko karibu na Chuo Kikuu cha
Makerere, Kampala nchini Uganda kuporomoka.
Wanafunzi
wa Chuo cha Makerere waliongea na EagleOnline kuwa, tukio hilo
lilitokea jana Jumatatu Aprili 11 mchana ambapo jengo hilo la Kyaseka
Towers lililopo barabara ya Makerere Hill karibu kabisa na chuo hicho
liliporomoka baada ya kuzidiwa urefu kwa kuwa mmiliki wake aliamua
kuongeza floor nyingine juu bila kibali kutoka mamlaka za ujenzi.




0 comments:
Post a Comment