Wednesday, April 27, 2016

Msanii Kala Jeremiah, baba 'Alama'
Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Kala Jeremiah ambaye kwa sasa anafanya poa na kazi yake ya 'Malkia' amebahatika kupata mtoto wa kwanza wa kiume siku ya Jumamosi usiku.

Kala Jeremiah ameonesha furaha kubwa kuweza kupata mtoto wa kwanza mwanaume na kusema anajisikia furaha na amani kuona kwa sasa ana familia yake.
“Siku ya Jumamosi tarehe 23/4/2016 majira ya saa 12:34 jioni Mungu alinibariki mtoto wa kiume, hakika ni furaha kubwa kwangu na kwa familia yangu. Mungu ni mwema sana. Haleluyah‬ ‎mtoto wa kwanza‬ ‎mtoto wa kiume" Aliandika Kala Jeremiah.
Baada ya siku kadhaa kupita Kala Jeremiah ametaja jina la mtoto wake wa kwanza na kusema anaitwa 'Alama' na yeye kujitambulisha kama baba 'Alama”

0 comments:

Post a Comment