Thursday, April 14, 2016

 https://scontent-mad1-1.xx.fbcdn.net/hphotos-xaf1/v/t1.0-9/13012819_1520878794888391_7663677203415175149_n.jpg?oh=0cf08981fe7f0557b1f407240a3c4136&oe=578440AF
SUMAYE
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alisema Kilango hakuwa na hatia kiasi hicho kwa sababu bado hajaujua vizuri mkoa huo.“Ukweli haiwezekani RC asimamie jambo hilo muda mfupi na hata akipewa miezi sita akakague watu hao ‘physically’ bado haitoshi.

“Kama aliletewa taarifa kuwa kuna watumishi hewa na yeye akasema hakuna…hapo kuna tatizo. Lakini ndio hivyo kila mtu na utawala wake, kumwajibisha mtu ambaye hata huo mkoa na ofisi hajaijua vizuri kwa kweli inasikitisha. Hii haijapata kutokea popote na si kitu cha kawaida,”alisema Sumaye.

2 comments:

  1. kweli kabisa hata mimi namuunga mkono sumaye,ni mapema mno na haraka kuadhibiwa bila kujua mkuu wa mkoa ana uzoefu gani na huo mkoa. inawezekana kuwa mama naye hakuona sababu ya kujiridhisha hilo linaweza kuwa shida yake kuu ila alistahili second chance. hivi kweli ujasiri na uchapakazi wote ule wa mama kilango leo anakuja kuonekana hivyo? eti muongo? ila waswahili wanasema likuepukalo lina heri nawe, tulia mama kama ipo ipo tu. nahisi nimeandika sijui kutokana na mapenzi yangu binfsi kwake labda kama mwanamke mwenzie. nimejistukia

    ReplyDelete
  2. YA SUMAYE NI ZIRO TUPU,NDIYO MAANA WAKATI WAKE ILIKUWA KULINDANA TU,ALICHOFANYA JPM NI SAHIHI KABISA HAKUNA CHA MUDA MFUPI,MKUU MZIMA WA MKOA UNAENDA KUTANGAZA UONGO,BILA KUHAKIKI HIVYO INA MAANA HAKUWA ANAFAA KWENYE HICHO CHEO

    ReplyDelete