Khadija Kopa amesema kinachosabisha wanawake kutosaidia wenyewe kwa wenyewe ni ‘nyodo’ ambapo amedai hata akienda hospitali ni bora atibiwe na daktari wa kiume kuliko wa kike.
Akizungumza katika kipindi cha Wanawake Live cha East Africa Television, Khadija amesema wanawake wengi hawapendani wenyewe kwa wenyewe.
“Unajua wanawake mara nyingi wananyodo hicho ndio kitu ambacho mimi mpaka leo napenda kutibiwa na madaktari wanaume, yaani mimi sindano nataka kuchomwa na mwanaume, hata kuzalishwa siku zote mimi nazalishwa na madaktari wa kiume sababu wanawake hatupendani” alisema Khadja Kopa.
Lakini mbali na hilo Malkia huyo wa mipasho aliwasii wanawake kupendana wao kwa wao ili waweze kupiga hatua mbele zaidi na kusema kitendo cha kutopendana kinawakwamisha kupiga hatua kimaendeleo na kujenga chuki kati yao.
“Unajua sisi wanawake hatupendani, mimi hapa ni mwanasiasa hivyo hata nikigombea nafasi fulani nitapata kura nyingi zaidi kutoka kwa wanaume na si wanawake, lakini ningependa leo niwaambie tu hata ukimkuta mwanamke wenzako anagombea nafasi fulani muoneshe support ya moja kwa moja, jamanii tunabidi tupendane” alisisitiza Khadja Kopa
0 comments:
Post a Comment