Monday, April 11, 2016

Ni jinsi gani Zanzibar huibiwa mapato kutoka kwenye sekta ya utalii .?


Ok!! This is how it works.

Kwa mfano muitaliano anajenga hotel kubwa Zanzibar madharani eneo la Nungwi. Wakati huohuo anafungua kampuni nyingine pale Panama au Isles of Man yenye undugu na hotel yake iliyoko Zanzibar. Amefungua Panama kwa sababu kodi hakuna au ipo kiduchu sana.

Watalii au wateja wake asilimia kubwa wantoka ulaya, wata book hotel ya Zanzibar kupitia kampuni tanzu iliyoko Panama kwa $800 per night madharani. Wateja wakiwa wengi anawachukulia charter flight wanapelekwa Zanzibar moja kwa moja.

Sasa wale wateja au watalii wakisha tumia hoteli wanaenda zao makwao, huku nyuma hoteli iliyoko Zanzibar ina raise invoice na kuipelekea kampuni yake tanzu iliyoko Panama kutaka kulipwa. Hiyo invoice itasomeka kuwa hawa watalii au wateja walikuwa wakichajiwa $100 per night na si $800 per night kama walivyolipa kwenye kampuni tanzu iliyoko Panama.

Kwa maana hiyo hoteli ya Zanzibar kwenye financial report zake ita ripoti mauzo yenye pungufu ya $700 per night kwa kila kichwa cha mteja au mtalii.

Automatically mauzo yatakuwa pungufu sana by $700 na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar - SMZ kupitia ZRB zanzibar revenue board ama TRA wataishia kupata corporate tax ndogo sana, tu kwasababu mauzo yamepunguzwa sana kiasi Cha $700 per night kwa kila kichwa.

Kwa maelezo yangu hapo unaweza ona ni jinsi gani ilivyo ngumu kwa SMZ kunufaika na rasimali yake ya utalii. Hii inatumika na takribani mahoteli yote kule zenji hata kwenye mbuga za bara.

Hizo hotel hazitaishia hapo zitaanzisha foundations za kawaida ili kusaidia wakazi huku wakionyesha fedha zile zimepekwa kwenye foundations wakati hata hazifiki na wanakuwa tayari wamepunguza kiwango cha kodi zaidi kwasababu faida itazidi kwenda chini.

Next time nitaongelea juu namna gani zao la samaki linavyochukuliwa poa na jinsi ambavyo likichukuliwa serious Zanzibar itapaa, ukiachana na mafuta na gas zilizoko kisiwani humo.

Sioni sababu ya msingi sana kwanini hiki kisiwa kiwe kama kilivyo sasa, naamini wangekuwa mbali sana hawa ndugu zetu. Solutions za hii kitu zipo

0 comments:

Post a Comment