Saturday, April 23, 2016




JAFFO
Mwana FA ni mmoja kati ya wasanii ambao hawazikubali collabo na wasanii wa nje ya Tanzania.

Hata hivyo akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Mwana FA alisema 2Face Idibia ni msanii pekee aliyekuwa na ndoto za kumshirikisha.
“Nilikuwa natamani kufanya collabo na 2Baba Idibia, lakini hakuna connection yeyote na yeye kwahiyo itakuwa ngumu na siwezi kusema tena kama mipango hiyo kama ipo,” alisema.
“Hata hapa kwetu kuna wasanii hao wa kimataifa ikitokea kama kuna ulazima kufanya hivyo nitafanya nao tu wapo kina Vanessa na wengine wengi tu hapa nyumbani. Unaweza ukatumia hela nyingi kufanya collabo na msanii wa Nigeria lakini angalia ni show ngapi unapata huko Nigeria,” aliongezea.

CHANZO na Bongo5

0 comments:

Post a Comment