Posted by Williammalecela.com on Wednesday, April 20, 2016
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
yuko nchini China kwa ziara ya kikazi ya siku sita (6) iliyoanza Aprili
17 mpaka April 23, 2016. Ziara hiyo ya Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi inafuatia mualiko rasmi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha
Kikomunisti cha China (CCP) na Rais wa China Mheshimiwa
Xi Jinping. Akiwa nchini China, anatarajia kukutana na viongozi wa juu
wa Chama Cha CCP na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na
kufanya nao mazungumzo yanayolenga kuimarisha uhusiano kati ya CCM na
CCP na serikali za nchi hizo mbili ulioasisiwa na Baba wa Taifa Hayati
Julius Kambarage Nyerere na Muasisi wa Taifa la China Mwenyekiti Mao Tse
Tung.
Mhe Kikwete
anatarajia kutembelea Jimbo la Fu Zhou, jimbo ambalo Rais wa sasa wa
China amefanya kazi zake za siasa kwa miaka 18, zilizompatia umaarufu na
uaminifu kwa watu wa China na kupelekea kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa
CCP na Rais wa China. Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa CCM Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete ameongozana na wajumbe watatu wa Kamati Kuu Mhe
Abdallah Bulembo, Dkt Maua Daftari na Mama Zakhia Meghji. Pia
ameongozana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dkt Titus Kamani,
Mwenyekiti wa Wilaya ya Mkalama Dkt Charles Mgana na maafisa wawili wa
Ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi.
0 comments:
Post a Comment