
Msanii mkongwe wa muziki wa taarabu, Mzee Yussuf amesema ataachia kazi mbili mpya za muziki wa mchiriku ili kuwapa uhondo mashabiki wake wa uswahilini.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video ya wimbo, Hewallah aliyomshirikisha Vanessa Mdee, ameiambia Bongo5 kuwa ana idea nyingi za muziki ambazo zinamfanya akifikirie kuziwakilisha kwa aina tofauti na muziki wake.
“Unajua ukisikia mtu amebadilika utamkuta kwenye Bongfleva, lakini nataka kuchanya muziki wangu, nitaimba Kisingeli, yaani kuna kitu nimekiona unapoamua kuchanganya muziki wako, pia nina nyimbo mbili za Mchiriku, moja inaitwa Wabaya ni Watu, na nyingine inaitwa, Baba Mwenye Nyumba,” alisema Mzee Yussuf.
Aliongeza, “Hii ndio idea, lazima niziwakilishe hata ikawa kwa njia tofauti, na nizipeleke kwa watu ili waelewe mimi ni mwanamuziki naweza kufanya kitu chochote ili mashabiki wangu waridhike,”
0 comments:
Post a Comment